Wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi Tawi la Moscow mnaombwa mlipe ada ya CCM mwaka 2010. kulingana na katiba ya CCM sehemu ya pili, fungu la kwanza, ibara ya 12(2), Ada ni Rub. 50. Wanachama wote mnaomwa kulipa ada hiyo kwa katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM Tawi la Moscow Bw. Boniface Assenga bl. 6, 562, Tel. +79258696322. Kumbuka, yeyote ambaye hatalipa ada ya Uanachama wa CCM, atakuwa amejiondoa kutoka CCM kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi sehemu ya pili, fungu la kwanza, ibara ya 13(1)d. Hivyo mwanachama huyo atatakiwa kuomba upya uanachama.
Pia wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi wanaotaka kujiunga na umoja wa Vijana UVCCM wawasilishe majina yao kwa katibu wa UVCCM Bw.MAHAMOUD.O.MBAROUK Tel. +79258696321. Mchango kwa ajili ya kadi hizo ni Rub. 50 na ziwasilishwe kwa katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM tawi la Moscow au kwa Makatibu wa fedha wa UVCCM Monica Makupa Tel. +79268426271, Octavian Nyalali Tel. +79258241202.
Chama cha Mapinduzi Tawi la Moscow kinawatakieni heri ya sikukuu ya Wanawake duniani 08/03/2010
похожие новости:
0 comments:
Post a Comment