MAAZIMIO YA KIKAO CHA KWANZA CHA MKUTANO WA PILI WA BARAZA KUU LA UVCCM: 06/12/2009 “TAWI LA CCM MOSCOW”
Balaza kuu la Vijana wa CCM, tawi la la CCM –MOSCOW , katika kikao chake cha tarehe 6/12/2009 kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wake Nd. Chrispin Domisio Bakunda , kilifikia maazimio yafuatayo:-
1: Hoja ya tawi kujitegemea kiuchumi:- Uanzishwaji wa miradi na michango mbalimbali /harambe kwa wanachama wa CCM-Urusi, Ili kukizi mahitaji husika katika wakati muafaka.Wajumbe wamependekeza uundwaji wa kamati ya fedha na uchumi ya tawi , ikiongozwa na katibu wa fedha na uchumi-tawi akishirikiana na na idara ya fedha na uchumi UVCCM-Tawi,, katika kuratibu, na kubuni mikakati ya tawi kujitegemea kiuchumi, ili kupata uelekeo wa utekelezaji wake. Riport ya utafiti na mapendekezo yake yawasilishwe kitika vikao vinavyofuata, kwa ajili ya utekelezaji.
2: Mpango wa kunadi sera za CCM chini Urusi : Baraza limeridhia kuwa Mpango wa kunadi sera kwa wanachama na wasio wanchama ndani na nje ya Moscow(miji mingine) ni muhimu na itakuza uelewa kwa wanachama, hii ikiambatana na ufunguzi wa mashina ktk miji husika kulingana/ kukidhi idadi ya wanachama.
Baraza linatoa rai ya Uundwaji wa kamati ya sera na itikadi ikiongozwa na katibu wa sera na itikadi tawi+katibu wa uhamasishaji na chipukizi –UVCCM ,kuandaa utekelezaji yaani kuanzaa mawasiliano na watu nje ya Moscow, kutafuta mbinu mbadala za kunadi sera za chama cha mapinduzi na majumuisho ya riport hiyo kuwasilisha na katibu wa sera na itikadi wa tawi vikao vya halmashauri kuu kwa ajili ya utekelezaji.
3: CCM-Moscow iwe na lengo la kusaidia jamii:- Tawi la CCM Moscow ,iwe jumiya itakayo toa kipaombele ktk kuwasaidia watanzania kulingana na matatizo yanayowakabili, hapa Urusi ikishirikiana na viongozi wa jumuia husika nje ya tawi, na hata Nyumbani Tanzania kwani Makundi mbalimbali ya kijamiii huko nyumbani yanahitaji misaada ya kiutu na kibinadamu. Wajumbe wanapendekeza Uundwaji wa mkakati yakinifu kutoka kwa wadau wenye mapenzi mema ikiwa pamoja na harambee ya kuwasaidia walio ktik mazingira magumu/maafa huko Tanzania.
4: Ongezeko la nafasi za wajumbe na Viongozi ndani ya UVCCM.:- Kulingana na uhitaji, na umuhimu wa idara mbalimabali za UVCCM pamoja na ujumbe , Na katika kukizi uwajibikaji wa kisekta husika kutokana na ukuaji wa Jumuiya ya vijana. Baraza la kuu la vijana limefanya Uteuzi wa makatibu wa idara nyeti za UVCCM TAWI, kwa kuzingatia kanuni za UVCCM.
Idara ya fedha na uchumi;- i) Octavian Nyalali- (katibu –fedha na uchumi –uvccm)
ii) Monica makupa (naibu katibu)
Idara ya Uhamasishaji na chipukizi :i) Kassim Koloa - (katibu wa uhamasishaji na chipikizi –uvccm).
ii) Ezelina Mwaifunga - (naibu katibu).
5 Taarifa na maoni :- katika hoja ya Usambazaji wa taarifa na ukusanyaji wa maoni toka kwa wanachama ndani ya mashina husika. Wajumbe wa vikao husika katika tawi wanatakiwa kushiriki kikamilifu bila woga wala aibu , wajumbe wa baraza wamependekeza kuwepo na mchakato wa kutoa taarifa za kiutendaji kwa makatabu wa idara husika njia ya website / email /simu.
6: Uwasilishaji wa Ajenda za vikao na maoni ya wajumbe : - wajumbe wameazimia kuwa sasa ni wakati muafaka wa kuendesha chama kisayansi zaidi , wajumbe wapate wasaa wa kupitia ajenda wiki moja kabla ya kikao, mjumbe kuandaa mapendekezo yake kimaandishi kulingana na ajenda husika ,kuwasilisha mtazamo wake kwa maandishi, au kwa email ya tawi/hoja binafsi wakati wa mkutano husika. Kwa kufanya hivi tutakua tunapanua demokrasia ya kimawazo ndani ya Tawi CCM hapa Urusi.
8:Uanzilishaji wa Kongamano:- Mradi wa kuanzisha kongomano la kisiasa /kijamii/kiuchumi/kiutamaduni , hasa katika sikukuu za ukumbusho wa waasisi wa chama na sikukuk za chama au sikukuu za kitaifa n.k. Uwasilishaji wa maoni kwa njia email, ushiriki ktk midaharo n.k.
Baraza limemtaka -katibu wa sera na uenezi tawi +idara ya chipukizi na uhamasishaji-uvccm kuleta mapendekezo jinsi ya utekelezaji azimio hili ktka vikao vinavyofuata vya tawi.
9: Kuitangaza Tanzania nchi za nje:-Baraza la vijana limetaka Vijana wote kujititokeza kikamilifu katika kusimamia mpango wa uhamasishaji katika shughuri za utamaduni na michezo kwani ndo njia pekeee ya kuitangaza Tanzania kwa mataifa mengine.
Baraza limemtaka -katibu sera na itikadi +idara ya chipukizi kuandaa hoja yakinifu katika utekelezaji wa Mradi huu.
10: Hafra ya Ugawaji Kadi za UVCCM: Baraza limepitisha kiwango cha rubu 50 kwa kila mwanachama, Ikiwa ni gharama za kuchangia gharama za hafra itakayo andaliwa siku ya sherehe za ugawaji kadi za CCM na UVCCM kwa wanachama wapya: Baraza linaitaka halmashauri kuu ya tawi kutoa Tarehe husika ya hafra hiyo ili maandalizi yaanze kutekelezwa mapema zaidi.
11: Adhabu kwa wajumbe wa vikao husika :- Adhabu za kinazamu /faini /onyo kutolewa kwa mjumbe ambaye hata udhuria vikao halali vya baraza la vijana vilivyotajwa bila taarifa siku moja kabla ya kikao. Atakaechelewa kuanzia dakika 30 baada ya kikao kuanza nakuendelea anatakiwa kutoa faini ya 50rub.
12: Demokrasia ndani ya chama:- katika Kukuza democrasia ndani ya chama wajumbe wamekubaliana kuwa ni wajibu wa mwanachama kushiriki katika kugombea nafasi ya uongozi iliyo wazi au wakati wa uchaguzi mkuu wa viongozi wa Tawi, ndani ya tawi kwa kufuata katiba ya CCM /kanuni ya UVCCM na mwongozo wa tawi.
13: Ufunguzi wa Website ya tawi { www.ccmmoscow.org } :-.Baraza linautaka uongozi wa juu wa tawi , kuharakisjha mchakato wa uzinduzi wa website ya tawi, ili kwenda sambaba na teknolojia ya kisasa ya habari na mawasiliano, ambapo wanachama popote walipo watakua na Uhuru wa kufuatilia / kuchangia maoni na mapendekezo yao kuhusu utendaji/shughuri za jumuia ya wanachama wa CCM .
14: Mkutano mkuu wa tawi: Wajumbe wa baraza la vijana wameridhia kuwepo kwa mkutano mkuu wa Tawi kwa wanachama wote waishio urusi mara moja kwa mwaka (majira ya kiangazi july-sept).
Taarifa za kiutendaji kwa mwaka uliopita kutolewa na katibu wa tawi, na Malengo na mipango ya baadae kuanishwa kwa maendeleo ya Tawi la CCM-MOSCOW.
…………………………………………………………………………
Imethibitishwa na :-
Mwenyekiti Jumuiya ya vijana –Tawi CCM-Moscow: 09/ 12/2009
похожие новости:


1 comments:
Makada wa ccm Ukraine tunawapongeza Tawi la CCM Moscow kwa mshikamano wenu.
Tunawaombea daima udumu.
From Emmanuel Japhet Kamara(ukraine)
Post a Comment