Dec 7, 2009

Yah: MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI TAWI LA URUSI

Yah: MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI TAWI LA URUSI
Wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya CCM Tawi la Moscow nchini Urusi mnatangaziwa kuwa , kutakua na Mkutano wa mwisho wa Halmashauri Kuu ya CCM Tawi la Moscow nchini Urusi Kwa mwaka 2009 ,

Mkutano huo Utafanyika tarehe 13/12/2009 siku ya jumapili, ukumbi wa mikutano wa block 6 –mikluho maklaya (moscow) , kuanzia saa 16:00-18:00.
Mkutano huo utaongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi –URUSI Dk. Alfred Kamuzora .

Ajenda za mkutano ni sita na zimeanishwa katika barua za mwaliko kwa wajumbe husika na kwa email zao. Pamoja na ajenda hizo kutakuwa na Uteuzi wa Katibu wa Tawi, Mwenyekiti wa UWT, na Katibu wa UVCCM.Kwa yeyote ambaye anapenda na anafikiri kuwa anaweza kushika nafasi hizo, anaweza kutuma maombi yake kwa mwenyekiti, katibu wa siasa na uenezi au kutuma barua pepe kupitia anwani ifuatayo; ccmmoscow@gmail.com. Jina kamili, namba ya simu, anwani na parua ni lazima vijumuishwe kwenye maombi hayo. Mwanachama yeyote halali wa CCM aishiye Urusi anaweza kushika nafasi mojawapo ya zilizotajwa hapo juu.

Wajumbe mnakumbushwa kuangalia email zenu na kupitia ajenda ili kujenga hoja yakinifu na zenye maslahi kwa tawi.

Fika bila kukosa.


похожие новости:

0 comments:


 
Авторские права 1996 - 2011 Chama Cha Mapinduzi. Haki zote zimehifadhiwa
.
Best Blogger Gadgets Best Blogger Gadgets